[...] "Ninapendekezo."Ilisonga mbele kama rafiki yangu April anapotaka kusema siri, ingawa hakuna yoyote kwa siri zake ni nzuri. Ama hata siri za Kweli. "usipoambia yeyote niko hapa, ninaweza kurekebisha macho yako." "Ondoka mjini!"
Iliwaka mara kadhaa. "Hicho ndicho ninachojaribu kufanya."
"Kile namaanisha ni kwamba huwezi kufanya hivyo!"
"Kwa nini?"
"Sawa, hakuna yeyote ameweza kurekebisha macho yangu isipokua miwani."
"Nina uwezo fulani.Utaona, mradi tu…”
"...Simwambii mtu yeyote kukuhusu?"
"Huo ndio moyo wake, hiyo ndio kivuli."
"Najuaje hutanifanya kipofu? unawezakua kama mmoja wa wale wauzaji wa simu ambao hutoa ahadi lakini ni za uongo kabisa."
Ilianza kung'aa, ikaacha tena. "Nisingefanya kitu kama hicho kwa kiumbe ambaye hajanidhuru."
"Kumaanisha ninge wahi kukudhuru, ungenifanya niwe kipofu?"
"Hilo ni kwa msingi wa kutaka kujua."
"Na ukirekebisha macho yangu, na nisiambie yeyote kukuhusu, utaacha mashamba yetu?"
"Huo ndio moyo wake!" [...]